Watu 20 wafa maji baada ya boti iliyobeba wahamiaji kuzama katika pwani ya Ugiriki
2022-11-03 08:32:32| CRI

Waokoaji nchini Ugiriki wamepata miili ya wahamiaji 20 waliokufa maji baada ya boti waliyopanda kupinduka na kuzama katika pwani ya Evia iliyoko Bahari ya Aegean jumanne.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la nchi hiyo AMNA, watu 12 wameokolewa wakati wa operesheni ya uokoaji, ambao wamesema kuwa watu 68 walikuwa ndani ya boti hiyo wakati ilipozama.

Msemaji wa Kikosi cha Ulinzi wa Pwani ya Hellenic, Kamanda Nikos Kokkalas amesema, wahamiaji hao wanatokea nchi za Misri, Afghanistan, na Iran.