Vikosi vya Serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray wakubali kusimamisha mapambano
2022-11-03 08:35:28| CRI

Serikali ya Ethiopia na kundi la waasi kutoka mkoa wa Tigray wamekubaliana kusimamisha mapambano baada ya siku kadhaa za mazungumzo yaliyofanyika huko Pretoria, Afrika Kusini.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na pande hizo mbili imesema, wawakilishi wa serikali ya Ethiopia na kundi la Harakati za Ukombozi wa Watu wa Tigray wamekubaliana kuwatangazia watu wa Ethiopia na dunia nzima kuwa baada ya mzungumzo ya siku 10, wamefikia makubaliano ya amani, ambapo watamaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mwili kaskazini mwa nchi hiyo.