Rais Xi Jinping anasisitiza umuhimu wa uwazi katika ustaarabu wa binadamu, ustawi wa dunia
2022-11-04 22:47:29| cri

Rais Xi Jinping wa China amesema uwazi ni nguvu kuu inayosukuma maendeleo ya ustaarabu wa binadamu na njia ya asili ya kuelekea ustawi na maendeleo ya kimataifa.

Rais Xi ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia kwa njia ya video sherehe ya ufunguzi wa Maonesho ya tano ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China.

Rais Xi amesema dunia ya leo inakabiliwa na mabadiliko ya kasi ambayo hayajaonekana katika karne moja iliyopita pamoja na kudorora kwa uchumi, hali inayohitaji nchi mbalimbali kujitolea kwa uwazi ili kukabiliana na changamoto za maendeleo, kuhimiza nguvu ya ushirikiano, kujenga kasi ya uvumbuzi, na kuleta manufaa kwa wote.

Rais Xi pia alitoa wito wa juhudi za kuendeleza mafungamano ya uchumi, kuongeza kasi ya ukuaji wa kila nchi, na kuzipa nchi zote fursa kubwa na ya haki kunufaika na matunda ya maendeleo.