Rais Xi Jinping asema China kubadilishana fursa na nchi nyingine kutokana na ushirikiano wa kina wa kimataifa
2022-11-04 21:07:02| cri

 

Rais Xi Jinping amesema China itashirikiana na nchi zote kuchangia fursa za ushirikiano wa kimataifa kwa pande zote.

Rais Xi ameyasema hayo alipohutubia kwa njia ya video ufunguzi wa Maonesho ya tano ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China.

"Tutashiriki kikamilifu na kwa kina katika mazungumzo ya mageuzi ya WTO, kuhimiza biashara na uwekezaji, na kuimarisha uratibu wa sera ya kimataifa ya mambo makuu ya uchumi, kwa nia ya kukuza kwa pamoja vichocheo vipya vya ukuaji wa kimataifa," alisema Rais Xi.

Rais Xi pia amesema China itajitahidi kikamilifu kujiunga na Makubaliano ya Kina na Maendeleo ya Ushirikiano wa Pasifiki na Makubaliano ya Ushirikiano wa Uchumi wa Kidijitali, ili kupanua mtandao wenye mwelekeo wa kimataifa wa maeneo ya biashara huria ya kiwango cha juu. China pia itaunga mkono kithabiti nchi nyingine zinazoendelea na kuzisaidia kukua kwa kasi, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi Jinping wa China amesema kufungua mlango ni nguvu kuu inayosukuma maendeleo ya ustaarabu wa binadamu na njia ya asiliya  kuelekea ustawi na maendeleo ya kimataifa.

Rais Xi amesema dunia ya leo inakabiliwa na mabadiliko ya kasi ambayo hayajaonekana katika katika miaka 100 iliyopita pamoja na kudorora kwa uchumi, hali inayohitaji nchi mbalimbali kujitolea katika kufungua mlango ili kukabiliana na changamoto za maendeleo, kuhimiza nguvu ya ushirikiano, kujenga kasi ya uvumbuzi, na kuleta manufaa kwa wote.

Rais Xi pia alitoa wito wa juhudi za kuendeleza mafungamano ya uchumi, kuongeza kasi ya ukuaji wa kila nchi, na kuzipa nchi zote fursa kubwa na ya haki kunufaika na matunda ya maendeleo.