Ubadilishaji wa obiti wa moduli ya majaribio ya Mengtian ya kituo cha anga za juu cha China wakamilika
2022-11-04 08:31:12| CRI

Shirika la Anga za Juu la China limesema, moduli ya majaribio ya Mengtian ya kituo cha anga za juu cha China imekamilisha kwa ufanisi ubadilishaji wa obiti Alhamisi saa 9:32 asubuhi kwa saa za China.

Ubadilishaji huo umeashiria uundaji wa kimsingi wa muundo wa T wa kituo hicho, ambayo ni hatua muhimu katika kukamilika kwa kituo cha anga za juu cha China.

Wafanyakazi wa Shenzhou -14 wameingia kwenye moduli hiyo jana alasiri.

Kwa mujibu wa mpango huo, vipimo vya msingi na tathmini inayohusika zitafanyika.