Msomi wa Ethiopia asema CIIE ni fursa kubwa kwa Afrika kupanua maeneo ya biashara ya nje
2022-11-04 08:30:04| CRI

Aliyekuwa mshauri wa kiuchumi katika Umoja wa Afrika (AU) na Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Costantinos Bt. Costantinos amesema, Afrika inapaswa kutumia maonyesho yajayo ya 5 ya Kimataifa ya Bidhaa Zinazoagizwa na China Kutoka Nchi za Nje (CIIE) ili kupanua maeneo yake ya biashara ya nje nchini China na katika soko la kimataifa.

Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua hivi karibuni, Constantinos amesema, maonyesho hayo yanatoa fursa adimu kwa kampuni za Ethiopia na nchi nyingine za Afrika kuingia katika fursa za soko nchini China na nchi nyingine.

Pia amesisitiza kuwa, wakati zikiboresha bidhaa za kilimo zinazouzwa katika soko la China, kampuni na serikali za nchi za Afrika pia zinapaswa kutafuta fursa za masoko mengine nchini China, licha ya bidhaa za jadi zinazouzwa nchini humo.