Kenya yatafuta nguvu ya teknolojia ya kiviwanda ya China katika maonyesho ya viwanda
2022-11-04 08:29:21| CRI

Kenya inayatumia Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Viwanda yanayofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, kutafuta nguvu ya teknolojia iliyoendelea ya kiviwanda ya China

Meneja Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji na Biashara katika Mamlaka ya Uwekezaji nchini Kenya (KenInvest) Pius Rotich amewaambia wanahabari kuwa, maonyesho hayo ni jukwaa la manufaa kwa kuwa yataonyesha mashine za China ambazo zinaweza kuongeza thamani ya malighafi za nchini Kenya.

Ametoa wito kwa kampuni za China kufanya uratibu na wawekezaji wa ndani ili Kenya iweze kupata teknolojia inayohitajika kutengeneza bidhaa kwa ajili ya soko la kanda ya Afrika mashariki na la kimataifa.