Wataalamu waunganisha milipuko ya magonjwa barani Afrika na mabadiliko ya tabianchi
2022-11-04 08:29:22| cri


 

Wataalamu wa afya barani Afrika jana wameunganisha kuongezeka kwa milipuko ya magonjwa barani humo na kuongezeka kwa matukio mabaya yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Meneja wa mambo ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO) anayeshughulikia mlipuko wa Ebola nchini Uganda, Bw. Patrick Otim jana amesema, kesi za Ebola na Kipindupindu zilizoripotiwa mwaka huu katika nchi kadhaa ni magonjwa yanayohusiana moja kwa moja mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema, katika miaka kumi iliyopita, zaidi ya asilimia 50 ya magonjwa yalilipuka katika miaka 5 iliyopita, ambapo mafuriko na ukame yamekuwa ni matukio ya kawaida, pamoja na kuongezeka kwa joto kutokana na mabadiliko ya tabianchi.