Rais wa Sierra Leone aishukuru China kwa msaada wa mashine za kilimo
2022-11-04 08:36:17| cri

Hafla ya kukabidhi msaada wa mashine za kilimo zilizotolewa na China kwa Sierra Leone ilifanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown, jumanne wiki hii.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais wa Sierra Leone Julius Bio aliishukuru serikali ya China na watu wake kwa kutoa msaada muhimu kwa ajili ya ujenzi wa kujitosheleza kwa chakula nchini Sierra Leone, akisema kuwa mashine hizo za kilimo zitakuza kilimo cha kisasa cha Sierra Leone na kuongeza uwezo wa uzalishaji wa chakula nchini humo.

Kwa upande wake, Balozi mdogo wa China nchini Sierra Leone Bw. Li Xiaoyong amesema, kilimo ni eneo muhimu la ushirikiano kati ya China na Sierra Leone, na China inapenda kuendelea kushirikiana na Sierra Leone kusukuma uhusiano kati yao kupanda ngazi ya juu