China yadhamiria kusaidia watu wa nchi na kanda tofauti kunufaika pamoja na internet
2022-11-07 11:24:00| CRI

Kwa mujibu wa waraka uliochapishwa leo Jumatatu, China imedhamiria kusaidia watu wa nchi na kanda tofauti kunufaika pamoja na internet.

Waraka huo uitwao “Kujenga Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja kwenye Mtandao” na kutolewa na Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China, umesema China inashikilia “Matumizi Bora ya Teknolojia” kwa kuwaweka watu mbele. Ikiitikia mahitaji ya  jumuiya ya kimataifa, China imeshirikiana na nchi nyingine kuziba pengo la kidijitali. Pia imehimiza mawasiliano ya kiutamaduni mtandaoni na kufundishana katika  staarabu za nchi mbalimbali pamoja na kuimarisha na kuunga mkono makundi ya watu wanyonge, na kusaidia watu wa nchi na kanda tofauti kunufaika pamoja na mtandao wa internet.

Huku ikitumia mtandao wa internet kuondoa umaskini wake, China imetumia teknolojia kusaidia nchi zinazoendelea kuboresha upatikanaji wa internet katika maeneo maskini zaidi na maeneo yenye watu wachache. Imefanya kazi kuhimiza upatikanaji wa mtandao wa internet kwa wote na kwa bei nafuu katika nchi zisizoendelea, ili kuondoa umaskini unaosababishwa na ukosefu wa vifaa vya internet.