Marais wa China na Madagascar watumiana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi
2022-11-07 12:25:30| CRI

Marais wa China na Madagascar watumiana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi.

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Madagascar Andry Rajoelina wametumiana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Katika salamu zake, rais Xi alisema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi miongo mitano iliyopita, uhusiano kati ya China na Madagascar umekuwa ukiendelea kwa njia nzuri na utulivu, bila kujali hali ya kimataifa inavyobadilika. Aliongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimeanzisha ushirikiano wa kina, na kuongeza  hali ya kuaminiana kisiasa na kuwasiliana na kushirikiana katika  sekta mbalimbali.

Xi alisema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Madagascar, na kwamba yuko tayari kushirikiana na Rajoelina kutumia maadhimisho hayo kama fursa ya kuendelea kukuza urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, ili kuleta manufaa kwa nchi mbili na watu wake.

Naye rais Rajoelina alisema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi miaka 50 iliyopita, Madagascar na China zimeimarisha urafiki na ushirikiano katika  sekta mbalimbali, jambo ambalo limekuwa na matokeo mazuri.