Jeshi la Somalia lawaua wanamgambo 21 wa al-Shabab
2022-11-07 10:20:59| CRI

Shirika la ujasusi na usalama la Somalia (NISA) limewauwa wanamgambo 21 wa kundi la al-Shabab na kuwajeruhi wengine zaidi 10 katikati ya nchi hiyo.

Wizara ya habari, utamaduni na utalii ya Somalia imesema operesheni ya usalama ilifanywa katika kijiji cha Galka Salimow baada ya shirika la ujasusi la nchi hiyo kupokea taarifa kuhusu mpango wa kundi la al-Shabab kufanya mashambulizi dhidi ya wenyeji.

Wizara hiyo imesema takriban wanamgambo 200 wa kundi la al-Shabab waliuawa wiki iliyopita katika mashambulizi ya mfululizo ya jeshi la Somalia.