Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenyekiti wa UNGA
2022-11-08 09:18:17| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alifanya mazungumzo kwa njia ya video na mwenyekiti wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) Bw. Csaba Korosi.

Bw. Wang Yi alisema China siku zote inaunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa na jukumu muhimu la UNGA, na itaendelea kushiriki katika ushirikiano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi  na kutoa mchango chanya kwa mafanikio ya mkutano wa COP27. Pia amesema China iko tayari kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta ya raslimali za maji pamoja na nchi nyingine kupitia utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo Duniani.

Bw. Korosi amepongeza kufanyika kwa mafanikio kwa mkutano wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kutarajia kuimarisha ushirikiano na China kufanikisha mkutano wa COP27.