Rwanda yakamilisha mashindano ya kung Fu
2022-11-08 08:58:33| CRI

Mashindano ya ubingwa wa Kung Fu ya Rwanda yalikamilika Jumapili mjini Kigali, ambako washiriki vijana wapatao 73 wasichana na wavulana waligombea nafasi kwenye fainali.

Mashindano ya awali yalifanyika kuanzia Oktoba 2 yakishirikisha mamia ya wachezaji vijana kutoka sehemu mbalimbali za Rwanda, na baada ya washindi kupatikana waliingia hatua ya fainali.

Balozi wa China nchini Rwanda Wang Xuekun amesema Kung Fu ni mchezo wenye manufaa kwa kila mtu ikiwa ni pamoja na vijana. Kupitia mazoezi makali na kupata ujuzi sahihi, anayejifunza anapata nidhamu ya ndani, busara na falsafa. Amesema Pia Kung Fu ina nafasi muhimu katika kuhimiza ushirikiano wa mabadilishano kati ya pande mbili na kuleta maelewano kati ya watu wa nchi mbili.

Mkuu wa Shirikisho la Kung Fu la Rwanda Bw. Marc Uwiragiye amesema Kung Fu ni moja ya shughuli muhimu zinazohimiza ushirikiano kati ya wachina na wanyarwanda.