Rais Xi Jinping apongeza maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Kimataifa ya Mianzi na Matete
2022-11-08 08:44:07| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Kimataifa ya Mianzi na Matete (INBAR) na Baraza la pili la Mianzi na Matete Duniani.

Kwenye barua yake, Rais Xi amesema tangu INBAR ilipoanzishwa, jumuiya hiyo imejitahidi kuendeleza uhifadhi, maendeleo na matumizi ya raslimali za mianzi na matete, na imechukua nafasi ya kiujenzi kwenye kuhimiza ulinzi wa mazingira na ikolojia duniani pamoja na maendeleo endelevu.

Amesisitiza kuwa China siku zote imeendelea na jitihada zake za kuhimiza maendeleo ya kiikolojia na kufuata falsafa ya maendeleo yenye masikilizano kati ya binadamu na asili.