Ethiopia yatoa tuzo kwa mfuko wa maendeleo vijijini wa China kutokana na miradi yake nchini Ethiopia
2022-11-08 08:59:27| CRI

Serikali ya Ethiopia imelipatia tuzo kwa Mfuko wa Maendeleo vijijini wa China kutokana na kazi zake za kutoa chakula mashuleni nchini Ethiopia.

Tuzo hiyo iliyoandaliwa na serikali ya mji wa Addis Ababa, imekabidhiwa kwa mfuko huo na Rais Sahle –Work Zewde wa Ethiopia.

Mfuko huo unatambuliwa kutokana na mchango wake katika kutoa chakula kwa shule moja ya Addis Ababa, na kupata tuzo ya Milan Pact inayohusu lishe endelevu kutoka miji 133 iliyotolewa mjini Rio de Janeiro. Addis Ababa ni mji pekee wa nchi ya Afrika uliopata tuzo kwenye mashindano hayo.

Kutokana na mafanikio hayo ofisi ya Meya wa mji wa Addis Ababa iliandaa shughuli ya kutoa tuzo ili kutambua mchango uliotolewa na wadau waliofanikisha mpango wa chakula mashuleni. Mfuko huo wa China umepata tuzo sambamba na Benki ya Dunia.