Kenya kutegemea uhifadhi wa misitu unaoongozwa na vijana kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi
2022-11-08 09:20:27| CRI

Serikali ya Kenya inapanga kuanzisha mipango ya uhifadhi wa misitu inayoongozwa na vijana ili kuimarisha uwezo wa jamii mashinani dhidi ya msukosuko wa tabia nchi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mistiu ya Kenya Bw. Joshua Cheboiwo amesema kwenye mkutano mmoja mjini Voi kwamba kushirikisha nguvu ya vijana kunatarajiwa kusaidia kufanya eneo la misitu lifikie asilimia 30 ya ardhi ya Kenya katika miongo kadhaa ijayo na kuharakisha mageuzi ya kijani.

Amesema eneo la misitu nchini Kenya ambalo kwa sasa ni asilimia 8.83 ya jumla ya ardhi ya nchi hiyo, linachangia asilimia takriban 3.6 ya pato la taifa kila mwaka ikitoa ajira laki 7.5 za moja kwa moja.