Umoja wa Afrika watoa mwito wa kuwepo uingiliaji ili kuhimiza maendeleo ya viwanda barani Afrika
2022-11-09 09:15:28| CRI

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Maendeleo ya uchumi, biashara, utalii, viwanda na madini Bw. Albert Muchanga ametoa wito wa kuwepo kwa uingiliaji ili kuhimiza maendeleo endelevu na shirikishi ya viwanda barani Afrika.

Kamishna huyo ametoa wito huo mjini Niamey nchini Niger kwenye mkutano wa pamoja wa mawaziri wa nchi za Afrika wanaoshughulikia viwanda na uchumi.

Amesisitiza haja ya kuunda taasisi za kutekeleza sera zitakazoweka mazingira wezeshi ya kibiashara yatakayorasimisha sekta binafsi, na kuboresha sera ya viwanda itakayohimiza maendeleo ya viwanda.

Pia ameongeza kuwa miundombinu na nishati ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda na hali mbaya ya upatikanaji wa umeme, maji, barabara na Tehama inatakiwa kuboreshwa.