Rais Xi Jinping wa China atuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa Kilele wa Mtandao wa Internet Duniani wa mwaka 2022 mjini Wuzhen
2022-11-09 14:01:18| cri

Mkutano wa Kilele wa Mtandao wa Internet Duniani wa mwaka 2022 umefunguliwa huko Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang, ukiwa na kauli mbiu ya "Kujenga Dunia ya Mtandao na Kuunda Mustakabali wa Kidijitali – Kushikana Mikono Kujenga Jumuiya yenye Hatima ya Pamoja katika Mtandao".

Akitoa barua ya pongezi kwa mkutano huo, Rais Xi Jinping wa China ameeleza kuwa katika zama za leo, teknolojia ya kidijitali, ikiwa ndio nguvu inayoongoza katika mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia na mabadiliko ya viwanda duniani, inazidi kutumiwa katika mchakato mzima wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kubadilisha sana mitindi ya uzalishaji na maisha pamoja na usimamizi wa jamii.

Ikikabiliwa na fursa na changamoto zinazotokana na mfumo wa kidijitali, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha mazungumzo na mawasiliano, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, na kufanya kazi pamoja ili kujenga mtandao wenye haki na wa kuridhisha zaidi, ulio wazi na jumuishi, ulio salama, thabiti na wenye kusisimua.

Xi Jinping amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine duniani ili kuendeleza kwa pamoja njia ya maendeleo ya kidijitali duniani inayojumuisha ujenzi wa pamoja na kunufaika pamoja na rasilimali za kidijitali, uchumi mzuri wa kidijitali, usimamizi sahihi na bora wa kidijitali, ustawi na maendeleo ya utamaduni wa kidijitali, ulinzi thabiti wa usalama wa kidijitali, na kufaidika kwa pande zote na ushirikiano wa kunufaishana wa kidijitali. Pia kuongeza kasi ya kujenga jumuiya ya mtandao wa internet yenye hatma ya pamoja na kuchangia busara na nguvu kwa maendeleo ya amani na ustaarabu wa binadamu.