China kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuhimiza usimamizi wa tabianchi duniani
2022-11-09 08:58:16| CRI

Kiongozi wa ujumbe wa China kwenye Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) Bw. Zhao Yingmin, amesema China inapenda kufanya kazi pamoja na jumuiya ya kimataifa kuhimiza utekelezaji wa pande zote, wenye uwiano na ufanisi wa Makubaliano ya Paris.

Akizungumzia ripoti kuhusu tabianchi na maendeleo nchini China iliyotolewa na Benki ya Dunia, Bw. Zhao Yingmin ambaye pia ni naibu waziri wa ikolojia na mazingira wa China, amesema China imetekeleza mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni changamoto na msukosuko wa pamoja unaowakabili binadamu, na siku zote imekuwa ikifuata kithabiti njia ya kutoa kipaumbele katika uhifadhi wa ikolojia na maendeleo ya kijani.