Tanzania kuongeza uandikishaji wa wanafunzi wa sayansi katika miaka saba ijayo
2022-11-09 09:14:49| CRI

Mamlaka za elimu nchini Tanzania zimesema zinapanga kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosomea sayansi kwenye taasisi za elimu ya juu kutoka wanafunzi elfu 40 kwa mwaka 2020 hadi kufikia wanafunzi laki 1.06 kwa mwaka 2026.

Naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia wa Tanzania Bw. Omary Kipanga, ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa idadi hiyo ya wanafunzi itaongezwa kupitia mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET).

Amesema kupitia mradi huo muhtasari wa masomo na mihadhara itakayotolewa kupitia mradi huo itapitiwa upya. Bw. Kipanga pia amesema jumla ya vyuo 14 vya elimu ya juu kutoka Tanzania bara na visiwani vitanufaika na programu hiyo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 425.