Wahanga 23 wa ajali ya ndege nchini Tanzania waruhusiwa kutoka hospitali
2022-11-09 09:51:14| CRI

Naibu waziri wa afya wa Tanzania Bw. Godwin Mollel amesema watu 23 miongoni mwa 24 waliookolewa katika ajali ya ndege iliyotokea Jumapili asubuhi kwenye Ziwa Victoria nchini Tanzania, wametoka hospitali, mwingine mmoja bado anaendelea na matibabu.

Bw. Mollel amesema rais Samia Suluhu Hassan ameagiza watu wote waliookolewa wapatiwe matibabu popote pale nchini kwa gharama za serikali.