Vijana wa Kenya waahidi kuunga mkono masuluhisho ya asili kwa dharura za tabia nchi
2022-11-10 08:58:28| CRI

Wanaharakati vijana wa mazingira wa Kenya wameeleza kuunga mkono mapendekezo yenye njia za asili yanayolenga kuimarisha uhimilivu wa jamii dhidi ya majanga mbalimbali yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwenye ufungaji wa mkutano wa siku tatu uliofanyika mjini Voi, kusini mashariki mwa Kenya, vijana hao wamesema wako tayari kuunga mkono mpango wa taifa wa kurejesha mazingira ya asili, ili kusaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kama mafuriko na ukame.

Mtunza mazingira mashinani Bw. Raymond Omondi kutoka Kaunti ya pwani ya Kwale, amesema vijana wako tayari kuleta mapinduzi kwenye ulinzi wa mifumo muhimu ya ikolojia kama misitu ya tropiki na ardhi oevu, ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa juhudi za Kenya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.