Barabara iliyojengwa na China yatajwa kuchangia ukuaji wa uchumi nchini Ethiopia
2022-11-10 09:33:40| CRI

Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC) imekamilisha mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 56.5 katika eneo la Oromia, Ethiopia, mradi ambao umefadhiliwa na serikali ya Ethiopia, na pia unahusisha ujenzi wa madaraja manne.

Baada ya kukamilika kwa barabara hiyo, mazao mengi ya mashambani kwenye eneo hilo ikiwemo ngano, shayiri na matunda, yatasafirishwa kwa urahisi zaidi na kufika kwenye soko la Addis Ababa kwa ubora wa hali ya juu na kwa kiasi kikubwa.

Pia barabara hiyo inatarajiwa kuhimiza utalii katika eneo la kusini-mashariki na kuvutia watalii wengi zaidi wa ndani na nje.