Xi Jinping kuhudhuria mkutano wa wakuu wa G20
2022-11-11 15:49:00| CRI

Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi za G20 utakaofanyika kuanzia tarehe 14 hadi 17 mwezi huu kisiwani Bali, Indonesia. Pia atahudhuria mkutano usio rasmi wa 29 wa wakuu wa APEC kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 19 mjini Bangkok, Thailand na kufanya ziara nchini humo.

Wakati wa mikutano hii, rais Xi atakutana na kuzungumza na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, rais Joe Biden wa Marekani, rais Macky Sall wa Senegal, rais Alberto Fernández wa Argentina na viongozi wa nchi nyingine.