Rais wa Sudan Kusini asisitiza kushikilia kanuni ya China Moja
2022-11-11 08:37:44| CRI

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema nchi yake itaendelea kufuata kithabiti kanuni ya China Moja, na inapenda kushikana mkono na China kutumia vyema fursa ya utekelezaji wa matokeo ya mikutano ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ili kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kati ya nchi hizo mbili na kuinua kiwango cha uhusiano wa pande mbili.

Akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa China nchini Sudan Kusini Bw. Ma Qiang, Rais Kiir ameishukuru China kwa uungaji mkono wake endelevu kwa amani na maendeleo nchini Sudan Kusini.

Balozi Ma Qiang amesema, China inapenda kuendelea kutoa msaada unaohitajika kadri inavyoweza kwa ajili ya mchakato wa amani wa Sudan Kusini, na kuendelea kuiunga mkono kithabiti Sudan Kusini kutafuta njia ya maendeleo inayofaa hali yake halisi.