Waziri wa mambo ya nje wa China atoa salamu za pole kwa mwenzake wa Tanzania kutokana na ajali ya ndege
2022-11-12 16:37:04| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ametoa salamu za pole kupitia simu kwa mwenzake wa Tanzania Bi Stergomena Tax kutokana na ajali ya ndege iliyotokea katika ziwa la Victoria. 

Bw. Wang ametoa salamu za rambirambi kwa waliofariki katika ajali hiyo na salamu za pole kwa jamaa wa waliofariki na waliojeruhiwa. Amesema,katika wakati huu wa kuhuzunisha,serikali ya China na watu wake watakuwa pamoja na ndugu wetu serikali ya Tanzania na watu wake.