Homa ya Ebola yaenea hadi mashariki mwa Uganda
2022-11-14 09:50:27| CRI

Wizara ya afya ya Uganda imesema homa ya Ebola imeenea hadi sehemu ya mashariki mwa Uganda kutoka katikati mwa nchi hiyo.

Waziri wa afya wa Uganda Bibi Ruth Aceng jana Jumapili alisema kupitia akaunti ya Twitter kuwa, mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 45 amethibitishwa kufa kwa homa ya Ebola Novemba 10 akiwa nyumbani kwake katika wilaya ya Jinja, mashariki mwa Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa ya Twitter ya Bibi Aceng, mgonjwa huyu alihusishwa na kaka yake aliyedhaniwa kuambukizwa ugonjwa huo, ambaye alisafiri kutoka Kampala hadi Jinja, na akafariki Novemba 3 baada ya kuumwa kwa siku 10 . Aceng aliongeza kuwa kazi ya kufuatilia watu waliokuwa karibu na mgonjwa na uchunguzi wa maradhi ya mlipuko imeanza kufanyika.