Mlipuko mbaya wa shambulizi la kigaidi watokea mjini Istanbul
2022-11-14 09:48:12| CRI

Makamu wa Rais wa Uturuki Bw. Fuat Oktay amesema kuwa mlipuko uliotokea katika barabara maarufu ya waenda kwa miguu mjini Istanbul umesababisha vifo vya watu sita na wengine 81 kujeruhiwa.

Amesema wanatathmini na kuona kuwa hiki ni kitendo cha kigaidi kilichofanywa na mshambuliaji mwanamke, na kusisitiza kuwa watawakamata wahusika wote, hata wakikimbia hadi ncha ya dunia. Miongoni mwa majeruhi 81 kuna wawili ambao wako mahututi.

Vyombo vya kutekeleza sheria viko katika hali ya tahadhari, na maafisa wa polisi wanalinda maeneo muhimu huku helikopta zikishika doria katika jiji hilo. Waendesha mashtaka watano wamepewa jukumu la kuchunguza mlipuko huo.