Xi Jinping:kutafuta mwelekeo sahihi wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani
2022-11-14 20:51:54| cri

Rais Xi Jinping wa China huko Bali,Indonesia amekutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden.

Rais Xi amesema,tangu China na Marekani kugusana,kuanzisha uhusiano wa kibalozi mpaka leo,uhusiano kati ya nchi mbili umepita miaka zaidi ya 50,ukipata mavuno na hasara,na kuleta uzoefu na mafunzo. Historia ni kitabu kizuri zaidi cha masomo. Tunatakiwa kujifunza kutoka historia na kukabiliana na siku za baadaye. Hivi sasa,hali inayoukabili uhusiano kati ya China na Marekani hailingani na maslahi ya nchi mbili na watu wao,pia hailingani na matarajio ya jumuiya ya kimataifa. Tukiwa viongozi wa nchi mbili kubwa,tunatakiwa kutafuta mwelekeo sahihi wa maendeleo kwa uhusiano huo,kuinua kiwango cha uhusiano huo. Wanasiasa wanatakiwa kufikiria na kuhakikisha mwelekeo wa maendeleo wa nchi,pia wanatakiwa kufikiria na kuhakikisha njia ya kuishi na nchi nyingine. 

Rais Xi amesisitiza kuwa hivi sasa,mabadiliko ya zama hii yametokea kwa njia isiyokuwepo zamani,jamii ya binadamu inakabiliwa na changamoto zisizokuwepo zamani,dunia inasimama katika njiapanda. Jumuiya ya kimataifa inatarajia China na Marekani kushughulikia vizuri uhusiano kati ya pande mbili. Mkutano wa leo unafuatiliwa na dunia nzima. Tunatakiwa kufanya juhudi pamoja na nchi mbalimbali kuimarisha matumaini kwa amani ya dunia,kuzidisha imani kwa utulivu wa dunia,kutia nguvu kwa maendeleo ya pamoja. Amesema,anaapenda kubadilishana maoni kwa udhati na kina na rais Biden kuhusu masuala ya kimkakati ya uhusiano kati ya pande mbili na masuala makubwa ya kikanda na kimataifa. Anatarajia kufanya juhudi pamoja na rais Biden kuhimiza uhusiano kati ya nchi mbili katika njia ya maendeleo yenye afya na utulivu,ili kunufaisha nchi mbili na dunia.