Mfululizo wa vipindi vya “Misemo ya Kale inayopendwa na Xi Jinping” (toleo la kiindonesia na kithailand)na documentary ya “China,Safari Mpya” zatolewa
2022-11-14 20:53:39| cri

Hafla ya utoaji wa Mfululizo wa vipindi vya “Misemo ya Kale inayopendwa na Xi Jinping” (toleo la kiindonesia na kithailand)na documentary ya “China,Safari Mpya” ya Shirika Kuu la Utangazaji la Taifa la China CMG imefanyika hapa Beijing. Mkuu wa shirika la CMG Bw. Shen Haixiong amehudhuria na kuhutubia katika hafla hiyo. Wakuu wa televisheni za taifa za Indonesia,Thailand,Combodia,India,Laos,Nigeria,Pakistan,Sri Lanka na Uturuki,na wakuu wa vyombo vikuu vya habari vya nchi hizo wamehudhuria hafla hiyo kwa njia ya mtandao.

Bw. Shen amesema,anatarajia utoaji wa vipindi hivi unawawezesha watu wa Indonesia na Thailand kuelewa kwa kina zamani,sasa na siku za baadaye za China ya zama mpya. Amesema,vyombo vya habari ni daraja la kufahamiana kwa watu wa nchi mbalimbali. Documentary ya “China,Safari Mpya” iliyotengenezwa na CMG na televisheni za taifa za nchi nane itatumia hadithi kadhaa kuwafahamisha watazamaji wa kigeni juhudi zilizofanywa na China katika kutimiza “usasa wa kichina”,kufichua siri ya China. CMG inapenda kushirikiana na vyombo vya habari vya nchi mbalimbali kuvumbua mtindo wa ushirikiano,kuimarisha undani wa ushirikiano,kuzidisha sekta za ushirikiano,ili kutoa mchango wa vyombo vya habari katika kuhimiza amani na maendeleo ya dunia,kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.