Serikali ya Ethiopia yasisitiza azma yake ya kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa hivi karibuni
2022-11-14 09:44:22| CRI

Serikali ya Ethiopia imesema kuwa inajitahidi kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyotiwa saini hivi karibuni ambayo yanalenga kumaliza mzozo uliodumu kwa miaka miwili kaskazini mwa Ethiopia.

Kwenye taarifa iliyotolewa Jumamosi baada ya makamanda wakuu wa serikali ya Ethiopia na Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) kukubaliana kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo yenye migogoro kaskazini mwa Ethiopia, Idara ya Mawasiliano ya Serikali ya Ethiopia ilisema juhudi zinafanywa ili kufikisha msaada wa kibinadamu katika maeneo mengi zaidi ya Tigray yaliyoathiriwa.

Pande za mzozo huo zimekubali kutozuia misaada ya kibinadamu kwa watu wenye uhitaji huko Tigray na mikoa jirani, na kuwezesha harakati za wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Afrika (AU).