Rais wa China awasili nchini Indonesia kuhudhuria mkutano wa G20
2022-11-14 15:52:06| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China leo alasiri amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ngurah Rai mjini Bali, Indonesia kwa ndege maalum, ambapo anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 17 wa kilele wa Kundi la Nchi 20 (G20) utakaofanyika Bali kuanzia tarehe leo tarehe 14 hadi 17.