Kampuni ya China kujenga jumba la biashara mjini Addis Ababa, Ethiopia
2022-11-14 09:45:48| CRI

Kampuni kubwa ya ujenzi ya China CCECC imesaini makubaliano na kampuni moja ya Ethiopia kujenga jumba la biashara mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mradi huo wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 200, ambao utajumuisha hoteli ya nyota tano, jengo la maduka na vyumba uliopo katikati ya mji wa Addis Ababa, baada ya kukamilika unatarajiwa kuhudumia idadi inayoongezeka ya wafanya biashara wanaosafiri, mashirika ya kimataifa na wawekezaji wa kigeni.

Ofisa mkuu mtendaji wa Kampuni ya DMC Trading Private, Dereje Habtamu alisema mradi huo utakaokamilika ndani ya miaka mitatu na nusu utakuwa moja ya alama za Ethiopia ambazo zitakumbatia teknolojia za kisasa za kiujenzi. Aliongeza kuwa sababu ya kampuni hiyo kuchagua CCECC ni kutokana na mafanikio yake katika kukamilisha kwa ufanisi miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo nchini Ethiopia, ikiwa ni pamoja na Reli ya SGR ya kutoka Addis Ababa hadi Djibouti.