Mji unaotumia teknolojia ya kisasa wa Kenya wawavutia wawekezaji wa China kupiga jeki sekta ya teknolojia
2022-11-15 10:19:17| CRI

Ofisa wa Konza Technopolis, mji unaotumia teknolojia ya kisasa wa Kenya, jana alisema kituo hicho cha teknolojia kinajitahidi kuwavutia wawekezaji wa China katika kuhimiza sekta ya teknolojia nchini humo.

Meneja wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na ufumbuzi wa mji wa kisasa huko Konza Technopolis Bw. Lucas Omollo alisema, kampuni ya teknolojia ya China Huawei imekamilisha ujenzi wa kituo cha data katika mji huo. Konza Technopolis inawapatia fursa wawekezaji wengine wa China katika kujiunga na mradi huo, ambao utainua hadhi ya Kenya ikiwa ni kitovu cha teknolojia cha kikanda.

Konza Technopolis ni mji wa teknolojia wa Kenya ulioko takriban kilomita 70 kusini mwa Nairobi, ambao unadhamiria kutumia teknolojia ya kisasa ya China kwenye sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mifumo ya kisasa ya usafiri wa umma, nishati endelevu, teknolojia ya kisasa ya akili bandia, teknolojia ya kifedha, ujenzi wa mambo ya digitali na teknolojia ya roboti.