Marais wa China na Ufaransa wakutana huko Bali
2022-11-15 11:04:30| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Bali, Indonesia.

Katika mazungumzo yao, rais Xi amesisitiza kuwa, zikiwa nguvu muhimu za dunia yenye ncha nyingi, China na Ufaransa na China na Ulaya zinapaswa kufuata moyo wa kujiamulia, ushirikiano na kufungua mlango, na kuhimiza uhusiano wao kuendelea vizuri na kwa utulivu.

Rais Xi amesema baada ya miaka mingi, China na Ulaya zimekuwa na uhusiano wa kutegemeana katika mambo ya uchumi, na zinapaswa kupanua biashara na uwekezaji, kudumisha utulivu wa mnyororo wa ugavi duniani, na kulinda utaratibu wa kimataifa wa uchumi na biashara. Amesisitiza kuwa China itaendelea kufungua mlango, na kutoa fursa mpya kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Ufaransa.

Rais Macron ameipongeza China kwa njia yake maalumu ya kujiendeleza, na kusema Ufaransa inajiamulia katika mambo ya kidiplomasia, na kupinga kupingana kwa makundi.