Rais wa China apendekeza kuhimiza maendeleo shirikishi zaidi duniani
2022-11-15 14:36:22| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China alipohutubia mkutano wa 17 wa kilele wa viongozi wa Kundi la Nchi 20 (G20) unaofanyika mjini Bali, Indonesia, amesema hivi sasa maendeleo ya binadamu yanakabiliwa na changamoto kubwa, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kuwa na mwamko wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu, kutetea amani, maendeleo, ushirikiano na mafanikio ya pamoja.

Rais Xi amesema zikiwa nchi kubwa, nchi wanachama wa G20 zinapaswa kubeba majukumu yao ya kutafuta maendeleo kwa binadamu wa nchi zote duniani. Amesisitiza kuwa kutofautisha nchi kutokana na mawazo ya kisiasa na kuanzisha makundi ya kupingana kutatenganisha tu dunia, na nchi zote duniani zinapaswa kuheshimiana, kutafuta maoni ya pamoja na kuvumilia maoni tofauti, kuishi pamoja kwa amani, na kuhimiza maendeleo ya uchumi unaofungua mlango duniani.