Rais wa China asema China inayoendelea kuwa nchi ya kisasa itatoa fursa zaidi kwa dunia nzima
2022-11-15 14:37:36| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China leo amehutubia mkutano wa 17 wa kilele wa viongozi wa Kundi la Nchi 20 (G20) unaofanyika mjini Bali, Indonesia.

Katika hotuba yake, rais Xi amesema Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimepanga malengo na sera kuu kuhusu maendeleo ya Chama na taifa, na China itashikilia kujiendeleza kwa njia ya amani, kukuza mageuzi na kufungua mlango zaidi, na kuhimiza ustawi mkubwa wa taifa la China kwa pande zote kwa kutimiza mambo ya kisasa kwa njia ya kichina. Ameongeza kuwa, China inayoendelea kuwa nchi ya kisasa itatoa fursa zaidi kwa dunia nzima.