Mkutano wa 17 wa kilele wa Kundi la Nchi 20 wafunguliwa kisiwani Bali, Indonesia
2022-11-15 11:03:51| CRI


 

Mkutano wa 17 wa kilele wa Kundi la Nchi 20 (G20) umefunguliwa kiswani Bali, Indonesia.

Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Ufufukaji Imara na wa Pamoja” utajadili mada muhimu zikiwemo miundombinu ya afya duniani, mageuzi ya kidijitali na mageuzi endelevu ya nishati.

Kundi la Nchi 20 ambalo lilianzishwa mwaka 1999 na wanachama wake ni pamoja na nchi kubwa za kiuchumi na masoko yanayoibuka, linachukua nafasi muhimu kwenye masuala ya kimataifa, na limekuwa moja ya mifumo ya pande nyingi yenye ufanisi katika kukabiliana na changamoto za kimataifa.