Rais wa China ahimiza nchi zilizoendelea kuzisaida nchi nyingine kupata maendeleo
2022-11-15 14:36:55| CRI


Rais Xi Jinping wa China leo amehutubia mkutano wa 17 wa kilele wa viongozi wa Kundi la Nchi 20 (G20) unaofanyika mjini Bali, Indonesia.

Katika hotuba yake, rais Xi amesema, kutokana na hali ya sasa, inapaswa kuhimiza maendeleo yanayonufaisha nchi nyingi zaidi duniani, kwani maendeleo ya kweli ni maendeleo ya nchi zote. Ameongeza kuwa, watu wa kila nchi wanataka kuishi maisha bora, mambo ya kisasa sio haki maalumu ya nchi chache, na nchi zilizoendelea zinapaswa kuzisaidia nchi nyingine kupata maendeleo.