Xi akutana na viongozi mbalimbali wa nchi na serikali huko Bali Indonesia
2022-11-16 10:10:13| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na viongozi mbalimbali wa nchi na serikali huko Bali Indonesia.

Alipokutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, Xi alisema katika miaka michache iliyopita uhusiano wa nchi hizi mbili umekumbwa na matatizo, ambayo nchi zote mbili hayapendi kuyaona, na kuongeza kuwa China na Australia ni nchi muhimu katika kanda ya Asia Pacifiki, hivyo zinapaswa kuboresha, kuulinda na kuupandisha ngazi uhusiano wa pande mbili ambao sio tu unatumikia kama maslahi ya kimsingi kwa watu wao bali pia unafaa kwa amani na maendeleo ya kanda ya Asia Pacifiki na dunia kwa ujumla. Naye Anthony Albanese amesema Australia iko tayari kushikilia ahadi iliyotolewa wakati pande mbili zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia, kushirikiana na China kwa moyo wa kuheshimiana na kuwa na ushirikiano wa usawa pamoja na kuondoa tofauti zao.

Rais Xi pia aliongea na rais wa Argentina na kumwambia kuwa, zikiwa nchi kubwa zinazoibukia kiuchumi, nchi hizo mbili zinahitaji kuwa na mtazamo wa kimkakati kwa kuweka muongozo wa kukuza uhusiano na kufanyaka kazi kwa ajili ya maendeleo ya kudumu katika ushirikiano wao wa kina na wa kimkakati.

Mbali na hao, rais Xi pia alikutana na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol na Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez.