Xi atoa wito wa kukabiliana kwa pamoja na changamoto za nyakati katika mkutano wa G20
2022-11-16 10:08:40| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema nchi zote duniani zikikabiliwa na changamoto, zinapaswa kukumbatia mtazamo wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutetea amani, maendeleo na ushirikiano wa kunufaishana.

Hayo aliyasema Jumanne kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 20 (G20) huko Bali, Indonesia, akizitaka nchi wanachama wa G20 kuongoza kwa mfano katika kuhimiza maendeleo ya mataifa yote, kuboresha maisha ya binadamu wote na maendeleo ya dunia nzima. Pia ametoa mapendekezo matatu akisema wanapaswa kufanya maendeleo ya dunia kuwa jumuishi zaidi, yanayonufaisha wote na yanayoweza kuhimili zaidi. Amesema wakati kauli mbiu ya mkutano wa Bali ni “Kufufuka kwa Pamoja, Kufufuka kwa Nguvu”, inatoa ujumbe mzuri kwa nchi za G20 kuwa na nia ya kuunga mkono ukuaji wa nchi zinazoendelea na kuzuia ufufukaji duniani ulio tofauti na usio na usawa.

Aidha rais Xi amezitaka pande zote kuendeleza ushirikiano wa kimataifa dhidi ya UVIKO-19, ili kuweka mazingira mazuri ya ufufukaji wa uchumi.