China yataka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi na kuongeza ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa
2022-11-16 10:12:12| CRI

Nchi zilizoendelea zinatakiwa kutimiza ahadi na kuongeza ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hayo yamesemwa na mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni mjumbe maalum wa China katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa Bw. Xie Zhenhua katika kongamano la ngazi ya juu la ushirikiano wa Kusini na Kusini kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa lililofanyika kwenye kikao cha 27 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa COP27 huko Sharm El-Sheikh nchini Misri.

Bw. Xie alibainisha katika hotuba yake kwamba nchi zinazoendelea ndizo waathirika wakuu wa mabadiliko ya hali ya hewa, wakikabiliwa na uwezo duni wa kukabiliana nayo na ukosefu wa msaada kutoka nje. Kwa upande mmoja, China inazitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi zao na kuongeza ufadhili wa hali ya hewa. Kwa upande mwingine, China inazisaidia nchi zinazoendelea kuinua uwezo wao kupitia ushirikiano wa Kusini na Kusini.