Peng Liyuan akutana na mke wa rais wa Indonesia
2022-11-17 09:04:00| CRI

Peng Liyuan, mke wa rais wa China Xi Jinping, jana Jumatano alikutana na mke wa rais wa Indonesia Iriana Joko Widodo.

Baada ya kuwasili, Peng alilakiwa na mwenyeji wake Iriana pamoja na vijana waliopiga muziki kwa ala ya jadi ya Kiindonesia, Gamelan. Akiambatana na Iriana, Peng aliangalia onesho la jadi la sanaa na utamaduni la Kiindonesia, pamoja na maonyesho ya bidhaa za ufundi. Mama Peng alimsifia sana mama Iriana kwa moyo wake wa kuleta ustawi wa umma na kumuelezea sera hai za China na mafanikio katika kutibu ugonjwa wa TB na Virusi vya Ukimwi, akisema anatarajia nchi mbili zitadumisha mawasiliano kwenye masuala ya ustawi na kuhimiza pamoja maisha ya watu.

Kabla ya kuondoka, wanafunzi wa Taasisi ya Confucius ya Utalii ya Chuo Kikuu cha Udayana cha Indonesia huko Bali, wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni, waliimba kwa Kichina wimbo wa Kiindonesia Begawan Solo.