China na Indonesia zakubaliana kujenga jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakabali wa pamoja
2022-11-17 09:02:19| CRI

Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo na Rais wa Indonesia Joko Widodo Jumatano jioni kisiwani Bali, ambapo wakuu hao wawili wa nchi walifikia makubaliano muhimu juu ya kujitahidi kujenga jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakabali wa pamoja.

Xi na Widodo walikubaliana kuchukulia maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya nchi hizo mbili yatakayofanyika mwaka ujao kama fursa ya kufungua matarajio mapya ya ushirikiano wa hali ya juu. Xi na Widodo pia walitazama kwa mara ya kwanza video ya majaribio ya reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung pamoja na video kuhusu mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Indonesia.

Kwa upande wake, Widodo alimpongeza tena Xi kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, akisema anatarajia pande mbili zitaimarisha ushirikiano wa kimkakati na wa kivitendo na kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya nchi mbili.