Mjumbe maalumu wa AU atoa wito wa kuongeza msaada wa kibinadamu mashariki mwa DRC
2022-11-17 09:30:25| CRI

Mjumbe maalumu wa amani wa Umoja wa Afrika Bw. Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kuongeza msaada wa kibinadamu kwa wakazi walioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako mapambano yamesababisha hasara kwa maisha na mali, na watu wengi kupoteza makazi yao.

Rais mstaafu wa Kenya, Kenyatta ambaye pia ni mratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeshughulikia Mchakato wa Nairobi juu ya Amani na Utulivu mashariki mwa DRC, alifanya ziara rasmi Jumanne huko Goma, mashariki mwa DRC, ambapo alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa wachukue hatua ya dharura yenye ufanisi, ili kupunguza mateso yanayowakabili watu.