Tarehe 2 Novemba ya kila mwaka ni Siku ya Kupambana na Uhalifu dhidi ya wanahabari duniani. Siku hii ni maalum katika kupambana na vitendo vya kihalifu dhidi ya wanahabari, ikiwa ni pamoja na kupigwa, kuuawa, kuharibiwa vyombo vyao, na uhalifu wa aina nyingine dhidi ya wanahabari.
Kwa muda mrefu sasa, wanahabari wanawake wamejikuta katika nafasi ngumu ambapo vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, kupewa kazi kutokana na jinsia, na aina nyingine nyingi za ubaguzi wa kijinsia ni changamoto ambazo wanahabari wengi wanawake wanakumbana nazo. Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake siku hii ya leo, tutazungumzia zaidi changamoto ambazo wanahabari wanawake wanakumbana nazo katika kutimiza majukumu yao.