Ethiopia yaanza kuiuzia nishati Kenya
2022-11-18 10:09:48| CRI

Shirika la habari la Ethiopia (EPA) jana liliripoti kuwa Ethiopia imeanza rasmi kuiuzia nishati Kenya.

EPA ilibainisha kuwa baada ya majaribio ya wiki moja, njia ya kusafirisha umeme yenye kilovolti 500 kati ya Ethiopia na Kenya ilianza rasmi kufanya kazi mapema Alhamisi. Njia hiyo ina uwezo wa kusafirisha umeme wa megawati 2,000 hadi sehemu ya mbali ya kusini Tanzania na nchi zilizoko kusini mwa Afrika.

Mradi huo wa kusafirisha umeme wenye thamani ya dola milioni 500 za kimarekani ulijengwa na kampuni mbili kutoka China na Ujerumani.