Xi asema China inaazimia kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja
2022-11-18 10:02:08| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kwamba China imeazimia kukuza ujenzi wa jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja, na itafanya zaidi ili kuimarisha utulivu na ustawi wa Asia-Pasifiki.

Xi ameyasema hayo katika hotuba yake ya maandishi, iliyopewa jina la "Kuendelea Kujitolea na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Kuleta Ushirikiano wa Asia na Pasifiki kwenye Ngazi Mpya”, kwenye mkutano  wa wakuu wa viwanda na baishara wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC).

Rais Xi amesema katika miongo kadhaa iliyopita, nchi za kanda hii zimekuwa zikitafuta maendeleo ya kiuchumi. Ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki umeleta msukumo mkubwa katika maendeleo ya kanda hiyo na kuboresha sana maisha ya watu wake.

Xi amesisitiza kwamba wakikabiliana na maendeleo haya mapya, ni lazima kuimarisha msingi wa maendeleo ya amani, kuwa na mtazamo wa maendeleo unaozingatia watu, kutafuta ufunguaji wa ngazi ya juu, kujitahidi kupata muunganisho wa hali ya juu, kujenga minyororo ya viwanda na ugavi imara na isiyozuiliwa na kukuza uboreshaji wa uchumi.