Xi akutana na vingozi wa Singapore na Ufilipino kando ya mkutano wa APEC
2022-11-18 10:03:26| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na viongozi wa Singapore na Ufilipino kando ya Mkutano wa 29 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC).

Alipokutana na Waziri Mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong, rais Xi amesema China inakaribisha ushiriki wa kina wa Singapore katika juhudi zake za kujenga dhana mpya ya maendeleo, na "ubora wa juu" unapaswa kuwa sifa kuu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Kwa upande wake Lee amesema ushirikiano baina ya China na Singapore unafurahia maendeleo makubwa, na kwamba kuinuka kwa China hakuwezi kuzuiliwa, na China yenye nguvu na urafiki italeta mchango mzuri katika kanda na dunia.

Alipokutana na rais wa Ufilipino Ferdinand Romualdez Marcos, rais Xi amesema anauangalia uhusiano wa nchi zao kwa mtazamo wa kimkakati na kwamba pande mbili zinapaswa kushikilia mashauriano ya kirafiki na kushughulikia tofauti na machafuko yao kwa usahihi.

Naye Marcos amesema Ufilipino itaendelea kutambua sera ya China moja, kanuni ya amani, na diplomasia huru, na haitachagua upande.